Saturday, April 7, 2018

KAULI YA MHE MBOWE KUHUSU KUKOSEKANA KWA MAONI YA UPINZANI BUNGENI

Hapa nitazungumzia mambo mawili muhimu, Kwanza kukosekana kwa maoni ya Upinzani Bungeni jana na pili uendeshaji wa kambi ya upinzani Bungeni, kanuni ya 16 (4) ya Bunge ndiyo iliyozaa kanuni za kambi ya upinzani, inaruhusu kambi kambi kutunga kanuni zake.


Bunge lina watumishi zaidi ya 400 lakini kambi ya upinzani inao wanne (4) tu, huu ni mkakati wa makusudi kuhakikisha kambi rasmi inakuwa under staffig, Watumishi wa upinzani walifukuzwa na Katibu wa Bunge mwezi Januari kutokana na mikataba kumalizika Desemba. Nilipomfuata Katibu wa Bunge kumuuliza kulikoni unawafukuza hawa watumishi kama mbwa? akanijibu anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni.


Ajira zao watumishi msubiri Spika, hadi leo kambi haina hata mtumishi mmoja, hatuna hata mtaalam mmoja wa kuandaa hotuba na kuchambua nyaraka. Sasa kwa hali hii tunapata wapi taarifa ya kuwasilisha Bungeni? Watumishi wa Ccm hapa Bungeni wapo na hawajafukuzwa kama wa kwetu.


Alitegemea mimi niandae hotuba Segerea ambako hakuna sekretarieti? Mikakati ya Katibu wa Bunge ni kuua upinzani, ndiyo jukumu alilokuja nalo, baada ya kuona kuna tatizo kwa Katiba, nilimwambia Spika anipatie kibali cha kuajiri lakini kanipa cha ajira 3, hivi kweli watumishi watatu wasimamie wizara zote? Tangu Januari nimenyimwa hata derev, tangu Janauri sijatumia gari hilo la Kiongozi Upinzani Bungeni (KUB) na hawanipi stahiki zangu ambazo zipo kisheria.


KWANZA - Hatutakuwa na hotuba za upinzani katika Bunge hili la Bajeti hadi pale watakaporuhusu kuajiri.


PILI - Hatutakubali hotuba zetu kuhaririwa.


TATU - Katibu wa Bunge afahamu upinzani ni watumishi wa watu na wameletwa Bungeni na watu.

No comments:

Post a Comment