Friday, October 6, 2017

Mauaji na Utekaji Tanzania: CHADEMA walia na Serikali, Lema, Masha na Kigaira walaumu IGP Sirro na Magufuli



John Mrema: Leo ni siku ya 29 tangu Lissu afanyiwe jaribio la kumuua, lakini mpaka sasa Polisi hawajaeleza Chochote wala hawajamshikilia Popote. Polisi walisema wameshikilia Nissan nane lakini wamiliki hawajulikani na Zilipo hapajulikani kwani hatujawahi kuziona.

John Mrema: Viongozi wa CHADEMA wanazidi kufuatiliwa na wa tu wasiojulikana. Wabunge Bulaya, Nassari, Lema, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Victoria Ngurumo, wote wametishwa na watu wasiojulikana. Lissu alitoa taarifa kwamba anafuatiliwa na watu wasiojulikana na baadae akashambuliwa.

John Mrema :" Ester Bulaya ametoa taarifa ametoa taarifa anafuatiliwa na watu wasiojulikana na wamemfuata mpaka nyumbani kwao Bunda" John Mrema

John Mrema: Leo tumewaita ili tuwaeleze kwamba huu mtiririko wa haya matukio inazidisha hofu na maiti 17 zilizopatikana Coco beach zinazidishaa hofu na Polisi polisi wanatoa majibu mepesi. Polisi wanadai Maiti zimetoka Angola na Msumbiji.

Sasa anaongea Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganizesheni Chadema Taifa, Benson Kigaira.

Kigaira: Kupitia nyie wanahabari tunawafikia watanzania. Tunataka tuzungumzie kuhusu hawa watu wasio Julikani na jinsi Polisi wanavyolishughulikia hili swala ndo maana tunasema na kuamini Serikali inahusika. Naomba muelewe hakuna aliye salama.

Kigaira: Lissu alitoa taarifa kuhusu kufuatiliwa kwake, na kuna kijana kwenye mitandao ya Kijamii alikuwa anaomba apewe Ruhusa yakumuua Lissu kwa Mikono yake. Baadae Lissu alipigwa risasi wala hajahojiwa. Baada ya Lissu Kupigwa risasi, akapost tena kwamba anasikitika sana kwa mtu aliyefanya hilo tukio la kumuua Lissu alitegemea asikie Lissu amekufa. Akasema wanamsubiri arudi safari hii hawatamkosa. Kwanini Polisi hawamuoni? Kwanini jicho la Polisi linachagua watu wa kuona? Kwanini Mtu akimkosoa Rais Magufuli unakamatwa jioni yake?

Kigaira: Hizo Nissan zilizokamatwa Polisi walizikuta Porini? mbona wamiliki wa hizo gari hawakamatwi? Ni kanyabonya wanataka kutudanyanya.

Kigaira: Mwigulu Nchemba alisema gari lililokuwa linamfuatilia Lissu lipo arusha halijawahi kukanyaga Dar es Salaam. Anatumia chombo gani kujua gari limefika sehemu fulani? Kama nacho hicho chombo basi anajua gari gani lilihusika kumpiga Lissu. Kwanini wenye gari wanatetewa? Huyo mtu anatuhumiwa, alitakiwa wamkamate yeye ndo aseme gari halijawahi kufika dar, kwanini mwigulu anamsemea? Hawa watu wanahusika.

Kigaira: Miili inayookotwa pale Coco beach hatujui ni ya nani na hatujui kama kesho wewe hautaokotwa Coco Beach. Polisi wanatakiwa watuambie na rais anatakiwa ajue, kama hajui hata yeye hayupo salama. Usalama wake nani anamhakikishia, kama hawana mashaka wanajua.

Kigaira: Polisi wanasema tumesimamisha upelelezi wa Lissu sababu Dreva hajapatikana. Je Dereva angekufa upelelezi usingefanyika? Dreva alikuwa ndani na risasi zimetoka nje. Pale getini kuna walinzi wanne wa Suma JKT siku ile walikuwepo wawili, na wao ndo waliruhusu gari liingie na baada ya kuingia waliruhusu gari likatoka, walishaulizwa?

Pale kwa naibu spika kuna Walinzi wenye silaha, kwanini hawakuipiga gari hata kwenye matairi, Risasi walizisikia. Kabla ya kumtafuta Dreva, hawa walinzi wapo wapi? kwanini hawahojiwi? wanamtaka Dreva. dreva anatibiwa, wanaweza kumfuata wakitaka. Lakini hawawezi kuacha upelelezi kisa Dreva hayupo.

Kigaira: IGP Sirro anataka kulitumia Jeshi la Polisi kisiasa. Mtu aliyemtishia bunduki Nape miezi kadhaa iliyopita, Kesho yake baada ya tukio lile, Polisi wakasema yule mtu sio Polisi, Wakati fulani Waziri wamambo ya ndani alisema alikuwa Polisi alishakamatwa na baadae akasema hajakamatwa. Leo Sirro anaomba watu wamsaidie kumjua mtu aliyemtishia Nape Bastola. Sirro hajamwambia aliyekuwa RPC wa Kinondoni Salome Kaganda aliyekuwa akiongoza Askari kumkataza Nape asifanye mkutano. Polisi walimuona hawakumkamata na leo wanaomba msaada wa kusaidia Polisi wamkamate.

Kigaira: Picha zipo, na jana watu walimtumia Sirro Picha nyingi sana, kwamba Wewe Sirro ambaye unasema Huyo mtu humjui, huyo hapo ni Bodyguard wa Makonda, lakini hajamtafuta.

Kigaira: Baada ya Video ya Rushwa iliyooneshwa na Lema na Nassari, Jerry Murro alisema "Nitashangaa sana kama vyombo vya dola vitaachia hili jambo lipite. Watu kama hawa wakina Nassari na Lema walitakiwa wapotezwe kabisa. Anashangaa Polisi halijawapoteza hawa watu. Kwanini Polisi haiwakamati watu kama Jerry wanaotishia amani ya Nchi? Kwanini hawawahoji?

Kigaira: Kwenye kikao cha ALAT cha juzi, baada ya hotuba ya rais, Mameya na Wakurugenzi waliomba ijadiliwe, lakini mwenyekiti wa ALAT alisema amepata maelekezo toka juu kwamba Hotuba hii haitakiwi kujadiliwa. Baadae kinyume na Utaratibu akaletwa mtu aliyejitambulisha kwamba yeye ni Mkurugenzi wa Oparasheni wa Jeshi la Polisi na akasema ameleta salamu za IGP kwenye Kikao cha ALAT. Akawambia yeye ndo anashghulikia vurugu zote, akasema hata watu waliopotea yeye ndo anshughulika. Halafu akaondoka. Hii ina maana alienda kuwatisha. Inawezekanaje Serikali aende kutisha kikao? tukisema Serikali inahusika, wanasema tunafanya uchochezi. Sisi tunaongea hali ilivyo, hali hii sio ya kitanzania.

Sasa anaongea Godbless Lema Waziri kivuli wa mambo ya ndani.

Lema: Kwa bahati mbaya sana tuna IGP anafikiri kuwa Kamanda mkakamavu ni kubeba silaha, Kamanda wa kweli sio Mtu mwenye silaha nyingi kwenye ghara bali ni mtu anayeweza akaconfront the truth hata mbele ya Boss wake.

Lema: IGP ni cheo kikubwa sana, jana mumeona IGP anaappeal kwa Public anaomba taarifa kwa raia wema ya mtu ambaye anamjua yule bwana ambaye anamjua aliyemtishia Nape Bastola. Kwa kauli sensitive kama ile, tungekuwa na nchi yenye good governance, IGP na Mwigulu leo wasingetakiwa kuwepo kazini. Baadae tunaona picha za huyo IGP anayeomba Msaada kwetu, tunamuona huyo mtu akiwa nyumba ya Makonda na IGP anamlinda IGP. Kama tuna IGP analinda Mhalifu, ina maana tanzania hii sio salama ya kuishi.

Lema: Wananchi wanaendelea kupoteza matumaini na jeshi la Polisi siku hadi siku, na hao wananchi wanaopoteza Matumaini ya jeshi la Polisi sio wajinga kwa kiwango hiki, sio wapuuzi kwa kiwangu hiki. Wasiwasi wangu hawa wananchi wakichoka,sifa tuliyonayo tanzania itapotea.

Lema: Jana tulimpelekea Picha nyingine Sirro ya Askari aliyekuwa akimvuta Nape kwenye gari sijui ni askari wa kikosi maalum, tukapeleka picha zote, tukamwambia hata huyu humjui ambaye amepiga picha hadharani? Sasa kama mkuu wa jeshi la Polisi anaweza kufanya hivi, hawa wadogo wakichukua maamuzi ya kudhalilisha watu kupiga watu na kuonea huko barabarani msiwalaumu kwa sababu wameshapata maelekezo kwa tabia za mkuu wa Jeshi la Polisi.

Lema: Ukiangalia tabia za Waziri Mwigulu, Sijui wanafanya nini ofisini, watu wanapotea, watu wanakufa na maiti zinaokotwa, nyie mnataka muwe sehemu ya wale watu, leo anatokea Waziri wa mambo ya ndani anasema wale inawezekana ni wakimbizi, Mkimbizi gani anauawa kinyama? Matishio yamekuwa mengi nchi hii.

Lema: Nilitekwa Makuyuni nikiwa na Mheshimiwa diwani Baranga, Nlipotekwa nlipiga simu kutafuta msaada wa RCO wa Arusha pomoja na Mwigulu, tuliweza kufanikiwa kukimbia na gari hadi sehemu walipokuwa Polisi, tukawaeleza na Polisi wakaenda sehemu ya tukio. Asubuhi nikapata taarifa kwamba Polisi walienda wakaua mtu mmoja kwenye hilo tukio. Inasadikiwa ni Miongoni mwa vijana 30 waliokuja kumteka mbunge wa Arusha Mjini.

Baadae nikapata baraka ya kwenda Magereza, nikiwa Magereza waliletwa vijana wengi walihusishwa na lile tukio. Nmekaa Magereza muda mrefu wakanisahau, Nikiwa Magereza Mbunge wa Babati Vijijini akaanza kuwafuatilia wale vijana walioitwa watekaji wa Lema.

Kumbe wale vijana waliopigwa risasi, walikuwa wanamfuatilia mtu aliyewaibia bodaboda. na huyo alouawa kauwawa kimakosa.

Polisi wakaanza kubembeleza familia imzike yule alopigwa risasi, ili aweze kuzikiwa walitaka wale waliokamatwa waachiliwe. Sijawahi kuona release order ikitoka mahakamani siku ya Jumapili kuja kutoa watu magereza, nliona siku ile. Manake lile tukio halikuwa la kijambazi ilikuwa ni hila kutuumiza maisha yetu.

Lema: tnachoappeal kwenu waandishi wa habari, kama Serikali inasema watu hawajulikani, basi Waziri na IGP hawatakiwa kuwa Maofisini.

Lema: Haya mambo yana mwisho, wakasikilize Redemption Song Lyrics - Bob Marley. Haya mambo yana mwisho


Lema: Yanafanyika darini, yatasitirika hadharani. Leo wanatuomba ushahidi. Huu mchezo unaoendelea, hawa vijana wanaliingiza taifa kwenye machafuko. Kilio cha watu kuuawa ni kilio cha watanzania wote wanaomheshimu Mungu. Kwanini Magufuli anarelax hawatafuti hawa watu?

Lema: Hawa watu wanafanya vitu viwili, moja kututishia tukae kimya lakini mbili mkikataa kutishiwa muuawe. wakitumaliza sisi watahamia kwenye makanisa ni Misikiti, ni rai yangu kwa wachungaji na Maaskofu, wasipigie tu kelele kwenye viroba, bali wapigie kelele na haya mauaji.

Lema: Magufuli ajue sisi pia tuna mwili na tuna damu na tuna ndugu. Hii hali imeanza kuleta matabaka.

Sasa anaongea Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha.

Masha: Nawakumbusha watanzania kazi ya jeshi la Polisi. Kazi yake kuu ni kulinda raia na mali zao pamoja na wageni wanaoingia bila kuangalia itikadi zao.

Masha: Ni vyema jeshi letu la Polisi litusaidie kupunguza hizi hisia.

Masha: Nlishangaa kuona Waziri wa Mambo ya ndani anakataa msaada wa uchunguzi kutoka nje ya nchi. Nikajua hawana nia njema. Sio jambo geni mbona viongozi wetu wamefanya training nje ya nchi? IGP aliyepita, kamanda wa Takukuru, Wambura wamefanya training Marekani. Kupokea msaada katika swala la uchunguzi sio aibu wala fedheha, hata Marekani wanaomba msaada kutoka nchi nyingine.

Masha: Namuomba rais awaagize makamanda wake watafute msaada, leo hii watanzania wanaishi kwa hofu.

Masha: Sisi watanzania maswala ya kiitikadi hajawahi kutusumbua wala udini. lakini sasa hivi watu wana hofu.

Masha: Juzi kati mzungu alosaidia nchi kupunguza uwindaji wa Tembo, alipigwa risasi akauawa.

Masha: Watu wanaogopa kutoka nje, watu wanaogopa kutembea usiku sasa hivi watu wanaogopa hata kuongea.

Masha: Waombe makamanda wako wapokea msaada wa uchunguzi sio fedheha.

Masha: Wananchi waendelee kumuombea Lissu na Viongozi wetu wote. Na serikali ifanye kazi inayopaswa kufanywa.

No comments:

Post a Comment