Friday, October 6, 2017

Bulaya: Nipo katika hatari kubwa, nimefuatiliwa na watu waliovalia kininja nyumbani

Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Ester Amos Bulaya, amesema yupo katika hatari kubwa kutokana na kufuatiliwa na watu ambao anahisi sio wazuri huku wakiwa wamevalia mavazi ya ninja, nyumbani kwake wilayani Bunda.

Bulaya ameto taarifa hiyo alipokuwa akiongea na mwandishi wa East Africa Television, na kusema kwamba watu hao walimfuata nyumbani kwake wakiwa na gari ya Noah huku wamevalia kinija, bahati nzuri hakuwepo nyumbani hivyo ndugu zake wakamwambia asirudi nyumbani siku hiyo.

Ester Bulaya ameendelea kuelezea kwamba watu hao walizunguka kwa baadhi ya ndugu zake akiwemo bibi yake na kumkosa, lakini alienda kutoa taarifa polisi na mkuu wa kituo kuanza kufuatilia suala hilo, lakini haikuchukua muda akahamishwa kituo cha kazi.


No comments:

Post a Comment