Friday, April 14, 2017

Tulaani sote tukio la Polisi kuuawa - Godbless Lema

Tukio la kuuwawa askari wa Jeshi la Polisi linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na kila Raia wa Taifa letu , hii ni dalili mbaya sana kwa ustawi wa amani ya Taifa letu . Hata hivyo ninamuomba Mungu awatie nguvu , ndugu , rafiki na familia zote za marehemu waliofikwa na msiba huu mbaya sana na mzito .

Polisi wameuwawa wakiwa kwenye wajibu wao wa kulinda raia na mali zao ni muhimu sasa kwa vyombo vya usalama kuwatia nguvuni na kuthibiti kwa weledi matendo kama haya yanayoendelea kushamiri kwa kasi sana , ni muhimu pia idara za ulinzi na usalama kufanya utafiti wa kina kujua ni nini haswa sababu za matukio kama haya.

Hatuwezi kuishi kwa amani bila ya kuwa na Jeshi la Polisi imara na ili tuwe na Jeshi la Polisi imara , tunapsawa kuwa na jamii inayotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi haswa kwenye nyakati ngumu kama hizi , hivyo ni matumaini yangu kuwa Wananchi wote hususani wa maeneo hayo yalipotokea mauaji watakuwa tiyari kutoa ushirikiano ili kuwabaini wahusika wa tukio hili baya.

Godbless Lema ( MB)
Waziri Kivuli Mambo ya Ndani.

No comments:

Post a Comment