Monday, October 31, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA



Kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 7.7.14 (g), Wabunge wa CHADEMA ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamefanya uchaguzi wa wajumbe 5 wa Kamati Kuu ya Chama, kuwakilisha kundi la wabunge.

Katika Uchaguzi huo uliofanyika Jumapili, Oktoba 30, mwaka huu, mjini Dodoma, wafuatao wamechaguliwa katika nafasi hizo;
1. Tundu Antipas Lissu
2. Godblesss Jonathan Lema
3. Joseph Osmund Mbilinyi
4. Ester Amos Bulaya
5. Mariam Salum Msabaha

Aidha, tunatoa taarifa kwa umma kuwa kutokana na Serikali kuamua kupuuza maoni ya wadau na wananchi kwa ujumla kuhusu kuongeza muda wa kujadili na kuboresha Muswada wa Huduma za Vyombo vya Habari, ambao iwapo utaachwa na kupitishwa kama ulivyo unalenga kutunga sheria hatari zaidi dhidi ya vyombo vya habari, haki ya wananchi ya kupata taarifa na hata uhuru wa kutoa maoni.

Kamati Kuu ya Chama katika kikao chake cha kawaida kilichoketi Oktoba 22-23, Jijini Dar es Salaam, pamoja na masuala mengine, iliazimia kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 7.7.16(p) kutuma ujumbe wa baadhi ya wajumbe waandamizi wa Kamati Kuu kwenda mjini Dodoma kukutana na Wabunge wa CHADEMA, ili kujadiliana na kutoa maelekezo ya Chama kuhusu muswada huo ambao unatarajiwa kuwasilishwa kwenye Mkutano wa Bunge unaoanza Jumanne, Novemba 1, mwaka huu.

Wajumbe walioteuliwa kuonana na wabunge ni;
1. Prof. Abdallah Safari (Makamu Mwenyekiti wa Chama Tangayika)
2. Prof. Mwesiga Baregu
3. Mh. Edward Lowassa
4. Mh. Frederick Sumaye
5. Mh. Arcado Ntagazwa

Imetolewa leo Jumapili, Oktoba 30, 2016 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

No comments:

Post a Comment