Tuesday, August 30, 2016

MASAA MATANO YA KUHOJIWA KINA MBOWE WAACHILIWA JIONI HII

Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni na mwenyekiti wa CHADEMA kamanda wa anga FREMAN MBOWE akizungumza na wanahabari baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya masaa matano Polisi Jijini Dar es salaam kwa kosa la kufanya mikutano ya ndani kinyume na agizo la POLISI.Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe amehojiwa Central Polisi kwa saa zaidi ya 5 na kutoka kwa.dhamana,akiwa na viongozi wakuu wengine walielekea Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam,leo Jumatatu.29/8/2016.

Viongozi waliokwenda polisi kwa mahojiano ni M/kiti wa Chadema Taifa, Mhe. Mbowe, Katibu Mkuu, Mhe. Vincent Mashinji, Mhe. Edward Lowassa, Mhe. John Mnyika,Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mhe. Said Issa Mohammed, Mhe. Tundu Lissu,Profesa Baregu ambapo walisindikizwa na Waheshimiwa Wabunge ambao walibaki nje wakiwasubiri, viongozi hao wametoka kwa dhamana na wametakiwa waripoti polisi tarehe 1 Septemba 2016


BAADA YA MAHOJIANO NA POLISI NA KUACHIWA KWA DHAMANA MBOWE ASISITIZA UKUTA UPO PALE PALE SEPTEMBA 1
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Mbowe baada ya kutoka Central Polisi kwa mahojiano na polisi na kwa saa zaidi ya 5 na kutoka kwa.dhamana,akiwa na viongozi wakuu wengine walielekea Makao Makuu ya Chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam,leo Jumatatu.29/8/2016.

Mbowe ameongea na wananchi waliojitokeza kumlaki baada ya kutoka polisi, amesisitiza kwamba UKUTA upo pale pale Septemba 1,2016, Maandamano na Mikutano ya hadhara yapo kwa mujibu wa sheria, hawavunji sheria yeyote huku akisisisitiza UKUTA upo pale pale.

No comments:

Post a Comment