Sunday, August 21, 2016

HOTUBA YA MHESHIMIWA FREEMAN MBOWE ALIPOKUWA KANDA YA KASKAZINI

Nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Afya ya kukusanyika hapa tena

-Kwa niaba ya chama napenda kutumia fursa hii kuwapongeza viongozi wa kanda ya Kaskazini kwa kazi kubwa mliyoifanya kipindi cha uchaguzi mkuu.
-Tumepata Madiwani,Halmashauri , Wabunge wengi na kura nyingi za Urais kuliko kipindi kingine chochote
- Mkoa wa Tanga hatujaweza kutoa mbunge lakini ndani ya Ushirikiano wa UKAWA tumepata Mbunge na Madiwani wengi.
Napenda kuwatia Moyo makamanda na wananchi wote wa Tanga .Naomba Mkutano huu uweke azimio maalumu la kuukomboa Mkoa wa Tanga kutoka kwenye makucha ya CCM

UJUMBE KWA TAIFA

-Tulipoamua Tarehe 1 Septemba iwe siku maalumu ya kuanza operesheni ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania(UKUTA) hatukupanga kwa nia ya kumjaribu mtu na kama kuna anayefikiria tunamjaribu Asubiri aone kwa kuwa tunapotetea na kulinda katiba na Sheria za nchi hatutamuogopa yeyote yule. Kamwe hatumuogopi!

-Rais na Wabunge wote waliapa,Waliapa kuilinda katiba ya nchi.

-Sisi kama Chama kikuu cha Upinzani ni kuangalia,Kuishauri na kuikosoa Serikali

-Wananchi hawakutupa dhamana ya kulea na kufumbia maovu hasa yale yanayokiuka haki za msingi za Kikatiba.Kamwe hatuwezi kuwa sehemu ya Wavunja sheria na katiba ya nchi

-Rais au Yeyote yule anapotoa Matamko yanayokinzana na Katiba,Tutamkatalia


-Rais Magufuli anatangaza kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020 .Utaratibu huu unakiuka Sheria za vyama vya siasa na katiba ya nchi.Sheria inatamka kuwa mikutano ya kisiasa ni haki ya vyama.Rais anaamua yeye anavyojua kinyume cha sheria eti Yeye peke yake na chama chake ndiye mwenye haki ya kufanya mikutano lakini sisi wengine tusubiri hadi 2020 ndipo tutekeleze haki yetu kikatiba na kisheria

Kwamba haki ya wengine inapoishia ndipo haki yake inapoanzia. Tutawaongoza wananchi kumkatalia,Hatumjaribu bali tunatetea haki ya wananchi kutoa maoni yao

MAAMUZI YA KAMATI KUU

-Uamuzi wa Operesheni hii ni uamuzi wa kikao halali cha Kamati kuu kilichoketi kwa siku 4 Mfululizo

kamati Kuu iliamua katika utekelezaji wa maazimio haya ,yaundwe makundi 5 maalumu yakiongozwa na wajumbe wa kamati Kuu

(i):Kundi la Kwanza linaongozwa na Prof.Mwesiga Baregu. Kundi hili lilipewa majukumu ya kujenga mahusiano shirikishi(Inclusiveness) ya ndani kama asasi za kiraia,makundi ya kidini,taasisi mbalimbali na Jumuiya ya kimataifa. Kwa kuwa Suala hili sio suala la CHADEMA pekee
(ii): Kundi la Fredrick Sumaye-Kwa ajili ya kushughulika na Masuala ya Kiserikali na Kibunge
(iii)Edward Lowassa-Kundi hili linajihusisha na upashaji habari kwa Umma
(iv): Kundi la Sheria litaongozwa na Tundu Lissu.
Kundi hili lenye wanasheria maahiri kabisa linaandaa mashitaka 21 katika mahakama za ndani kwenye kanda zote nchini,Afrika Mashariki na Mahakama za kimataifa
Tunataka Dunia ishuhudie jinsi ambavyo Utawala Wa Magufuli unavyojiandaa kuvunja haki za binadamu.

5-Kamati ya Maandalizi/Mikakati.Yaani kamati za kikanda

Viongozi wametapakaa katika kanda zetu zote

Mhe.Lissu na timu yake ya Wanasheria wamebaki Makao makuu kuandaa mashitaka na Shughuli za kisheria kuelekea Septemba Mosi

-Kuna watu wanafikiri UKUTA inaua UKAWA. Hatuna utengano na wenzetu wa UKAWA

Wenzetu CUF wanajiandaa na Uchaguzi Tarehe 21/08/2016 kumchagua Mwenyekiti Mpya

-Natumia fursa hii kwa niaba ya Chama Chetu kuwatakia kila la Kheri CUF katika uchaguzi huu wa viongozi wa kitaifa na pia kuwaombea heri
Mbinu za watawala zinazolenga kuwagawa Wana-CUF zitashindwa

-NCCR-Mageuzi tupo nao na pia Wiki Ijayo kutakuwa na kikao cha viongozi wakuu wa UKAWA kuhusiana na suala hili
Hata jana nilipotoka Dar Es Salaam nilikutana na viongozi wenzangu.Kwa hiyo ndani ya UKAWA hakuna shida yoyote kama ambavyo watawala na vyombo vyao wanavyojaribu jaribu kupotosha

-Hata Wana-CCM tunawakaribisha.Suala hili ni la Watanzania wote wanaochukia maovu

-Tulitarajia kuwa Rais Magufuli na chama chake angeweza kuwaomba vijana wa CCM(Kama wanao wa Kutosha) waingie barabarani kuwaunga wao mikono lakini badala yake ameona busara kutumia majeshi,kutumia vyombo vya Dola kuingia Barabarani

-Leo waliposikia tuna vikao wakaanza kusambaza vikosi vya polisi barabarani .Leo wamesambaza vikosi kila mahali
-Natumia fursa hii kuonya jaribio la kutumia askari hawa ambao ni ndugu zetu kulinda Uovu
-Septemba Mosi hatuendi,kupambana na Dola


-Kama ilivyo kwa madikteta wote,hata huyu anayetisha watu nae anahofu.Anataka kututia hofu kwa vyombo vya dola lakini sisi hatumuogopi kwani sisi tuna Mungu

-Natambua kuna wito wa viongozi wa Dini kutukutanisha.Hatukatai wito kwa kuwa tunawaheshimu.Tutawasikiliza na tutawaeleza msimamo wetu .

Magufuli ndiye anayevunja amani ya nchi hivyo viongozi wa Dini wamkanye kabla hali haijawa mbaya

-Tumeviandaa vyombo vya habari na vya kimataifa ili Septemba Mosi Dunia ishuhudie uovu wa Serikali ya Magufuli

-Tunajua hata baadhi ya Wana-CCM ni waathirika wa Uonevu Huu ,Wasio na vyama na wengine wote tunawakaribisha

Asanteni Wanahabari.Sasa tutaanza kikao chetu cha Ndani kwa mikakati kabambe

Tunawashukuru na Mwenyezi Mungu awabariki katika kazi yenu

No comments:

Post a Comment