Thursday, January 22, 2015

Freeman Mbowe atoa magari ya wagonjwa Hai

Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA, Mbunge wa Jimbo la HAI,,na Kiongozi wa kambi RAsmi bungeni MH FREEMAN MBOWE ameendeleza juhudi zake katika kuokoa maisha wa watu wa jimbo lake ambapo wiki hii ametoa ambulances kwa ajili ya watu wa jimbo lake....

Kutolewa kwa ambulance hiyo itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wakazi wa HAI jimbo ambalo limetawaliwa na mito na mabonde mbalimbali ambapo litatumika kuwawaisha wagonjwa hospitali za teule ya Machame na ile ya Wilaya.

Kufuatia kutolewa kwa ambulance hiyo mkazi mmoja wa kata ya Machame Mashariki(LYAMUNGO KATI) amesema itakuwa ni msaada mkubwa sana kwao maana itarahisisha kupeleka wagonjwa kutoka Kituo cha afya Lyamungo Hadi hospitali teule ya Machame.

Baadhi ya wakazi wa Masama(Masama Bweera) wameonekana kufurahia na wengine kudiriki kusema kama FREEMAN MBOWE atagombea tena watampa ushiindi wa kishindo kutokana na mheshimiwa Mbowe kutoa Ahadi zake bila kupendelea upande wowote.


No comments:

Post a Comment