Saturday, October 18, 2014

Chadema; Wakulima msikubali kudanganywa.na CCM.

na Bryceson Mathias, Morogoro.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewaonya Wakulima Morogoro, wasikubali kudanganywa na Siasa za Chama cha Mapinduzi (CCM), ili kumkopesha Mazao yao Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kwa ahadi ya kulipwa fedha zao baadaye.

Akizungumza na Gazeti hili Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Kihonda Maghorofani, Elizeus Rwegasira, alisema, kuna na Madai ya baadhi ya Vigogo wa Serikali wamejigeuza Wachuuzi wa Mazao hayo, hivyo NFRA inawapendelea kuwapa Magunia na kuwatosa Wakulima Walalahoi.

“Hali ya Wakulima walalahoi ni mbaya, hawajitambui kuwa wanaendelea kupewa Ulaghai na CCM bila kujua cha kufanya juu ya mauzo ya mazao yao. Chadema tunawashauri, Wanaweza kuuza kwa wanunuzi wa kawaida au kusubiri mwelekeo mzuri wa Mahitaji na Ugaviwa Soko.
“Msirubuniwe na wanasiasa uchwara Msisubiri Mahitaji na Ugavi wa Soko (Demand and Supply) Mtalia kilio kibaya, maana kinachoonekana sasa, baadhi yao wanatumia fedha ya Serikali ya NFRA kununua mazao yao, wajinufaishe wao na ndugu zao”.alionya Rwegasira.
Meneja wa Kanda wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Emmanuel Msuya, alikanusha NFRA kuwapa Upendeleo Vigogo wa Serikali Magunia ya Mahindi ili kubeba wao na ndugu zao wauze Mahindi yao, isipokuwa alidai wanaowapa ni Mawakala wao waliosajiliwa.

Kauli hiyo ilipingwa na Wakulima wakidai, Serikali ilishatangaza mahhindi hayawezi kuuzwa kwa Mawakala isipokuwa iyanunua moja kwa moja kwa Wakulima, jambo ambalo Viongozi wa NFRA wanakiuka kwa kuwapendelea vigogo kuwapa magunia wauze mazao yao.

“Utaratibu upo wazi, kwamba mahindi ya mkulima ndiyo yanapaswa kupewa kipaumbele, na Serikali imeliagiza hilo, lakini cha kushngaza mahindi ya Mawakala pamoja na wachuuzi ndiyo yanayopewa nafasi kubwa jambo ambalo hatukubaliani nalo kabisa”, alisema Mkulima aliyeomba asitajwe.

No comments:

Post a Comment